MACHI Mosi, Uwanja wa Taifa, KMC itakuwa na kibarua cha kumenyana na Simba mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
KMC ina kumbkumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru kwa kufungwa mabao 2-0 itakuwa na kazi ya kupindua meza kibabe.
Nyota wa KMC, Charles Ilanfya amesema kuwa kikosi kinajipanga kwa ajili ya mechi zote wana imani ya kupata matokeo.
"Mechi zetu kwetu ni muhimu kupata matokeo licha ya kutokuwa na mwendo mzuri, matumaini yetu tutarejea kwenye ubora na tutafanya kitu cha tofauti, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Post a Comment