MAMBO  bado si shwari ndani ya mtaa wa Jangwani kutokana na mdudu sare anayewaandama huku ikielezwa kuwa sababu kubwa ni kuwa na nyota wengi wa kigeni ambao Kocha Mkuu Luc Eymael bado hajawaelewa.

Yanga ikiwa imepata sare nne mfululizo imefunga mabao mawili ndani ya mechi hizo nne ambapo mchezaji wa kigeni aliyefunga ni mmoja na anaonekana kuwa na msaada ndani ya timu huku wengine mabo yakiwa bado.

Bernard Morrison, alifunga bao kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City pia alihusika kwenye pasi ya mwisho  mbele ya Polisi Tanzania kwenye sare ya kufungana bao 1-1 bao lililofungwa na Tariq Seif.

Imeelezwa kuwa ni nyota wanne wa kigeni bado Eymael hajawaelewa jambo linalomfanya asiwatumie mara kwa mara na wakishindwa kuwa bora panga halikwepeki kwao.

Wachezaji hao ni pamoja na David Molinga raia wa Congo ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa amefunga mabao manne ila kwa sasa amekuwa hatumiki.

Yikpe Gnamien mwili jumba ambaye usajili wake ulikuwa una sarakasi nyingi yeye ni raia wa Ivory Coast amefunga mabao mawili moja kwenye ligi mbele ya Singida United na lingine kwenye Kombe la Shirikisho ila mpaka sasa bado hajafurukuta.

Erick Kabamba raia wa Zambia yeye maisha yake bado hajawa na furaha kwani hana nafasi kikosi cha kwanza zaidi ya kuishia benchi kwenye baadhi ya mechi, Patrick Sibomana raia wa Rwanda ghafla tu amepotea kwenye ramani na kubaki akisugua benchi.

Habari zinaeleza kuwa usajili waliofanya kwa sasa unawagharimu kwa kukosa mtu sahihi anayeweza kufanya majukumu waliyokuwa wanahitaji.

Kocha Mkuu, Eymael alisema kuwa kikubwa kinachohitajika ndani ya kikosi ni wachezaji kuwa watulivu huku akifanyia kazi mapungufu yaliyopo ndani ya kikosi hicho

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.