PAUL Pogba kiungo mshambuliaji wa Manchester United amesema kuwa hapendi kuiona Liverpool ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Liverpool na Manchester United ni wapinzani wakubwa jambo ambalo linawaumiza United kuiona ikitwaa ubingwa kutokana na nafasi iliyopo kwa sasa.
Kiungo huyo ambae amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu amesema kuwa ni Manchester United ilistahili kutwaa ubingwa huo ila ilikosea kwenye kuanza jambo ambalo limewaweka kwenye wakati mgumu.
"Tulikuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa kwa kuwa tuna kikosi bora na tupo vizuri, kosa letu ilikuwa kwenye kuanza, naona Liverpool inapambana kutwaa ubingwa ila sipendi kuona ikitwaa ubingwa," amesema.
Liverpool ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 huku United ikiwa nafasi ya tano na pointi zake 41 zote zimecheza mechi 27.
Post a Comment