SHIZA Kichuya, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa kukaa nje muda mrefu bila kucheza mpira kumemponza asiwe kwenye ubora wake tofauti na zamani.
Kichuya amesema kuwa uwezo wake haujawa bora kutokana na matatizo aliyokuwa akipitia ambayo kwa sasa yameanza kumeguka taratibu na anarudi kwenye mfumo aliokuwa ameuzoea.
"Sijacheza mpira zaidi ya miezi mitano kutokana na mambo niliyokuwa ninapitia, jambo hilo ni sababu ya mimi kutokuwa bora ila haina maana kwamba sina kiwango.
"Kwa mchezaji ambaye hajacheza muda mrefu ina maana kiwango chake pia hakiwi kwenye ubora ule ambao wengi wanautarajia imani yangu nitafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa." amesema.
Kichuya amejiunga na Simba kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Klabu ya Pharco FC ya Misri jana alikuwa kwenye kikosi cha kwanza kilichocheza dhidi ya Stand United kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.
Simba ilishinda kwa mikwaju 3-2 ya penalti na kutinga hatua ya robo fainali baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90
Post a Comment