JANA Februari 26 kikosi cha Simba kilitua Dar kikitokea Shinyanga, leo kinatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa dhidi ya KMC.

Kwenye mchezo wao uliochezwa Februari 25 dhidi ya Stand United Simba ilitoshana nguvu na Stand United kwa kufungana bao 1-1 na ilipenya kwa ushindi wa penalti 3-2 zilizoipeleka jumla hatua ya robo fainali.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa makosa waliyoyafanya huko watayafanyia kazi ila leo wataanza maandalizi kwa ajili ya mechi zao zinazofuata.

"Tumemalizana na mtihani wa kwanza, tunatazama mechi zetu zijazo kwani mwisho wa mchezo mmoja ni maandalizi ya mechi nyingine, kikubwa ni kufanyia kazi makosa,",

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.