MACHI 27, timu ya Taifa ya Tanzania itakuwa na kibarua cha kumenyana na timu ya Taifa ya Tunisia utakaochezwa Uwanja wa Stade Olympique de Rades.
Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya Taifa Stars kufuzu michuano ya Afcon kwa mwaka 2021.
Kwnye mchezo huo waamuzi watatoka Angola ambao ni Helder Martins Rodrigues De Carvalho-Katikati -Jerson Emiliano Dos Santos-Msaidizi 1, Ivanildo Meirelles De O Sache Lopes-Msaidizi 2, Joao Amado Muanda Goma-Akiba.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Etienne Ndayiragije amesema kuwa ana matumaini ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo.
Post a Comment