YANGA imeweka rekodi ya kipekee ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa timu iliyofunga mabao machache kati ya timu zilizo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga imecheza mechi 22 imejikusanyia pointi 41 imefunga jumla ya mabao 25 huku kinara wake wa kutupia mabao ni David Molinga mwenye mabao saba.

Timu inayofuata kutupia mabao machache ndani ya nne bora ni Namungo iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43 imefunga mabao 29 na kinara wa kutupia ni Relliants Lusajo ametupia mabao 10.

Nafasi ya tatu ni Azam FC imefunga mabao 31 kinara wake ni Obrey Chirwa amefunga mabao nane na imecheza mechi 24.

Namba moja ni Simba iliyocheza mechi 24 imefunga mabao 50 na kinara wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao 14

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.