MABINGWA watetezi Simba kesho, Machi Mosi watakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na KMC mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa mabao 2-0 Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa kwanza msimu huu.
Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck imetoka kushinda mchezo wao wa Kombe la Shirikisho na kutinga hatua ya robo fainali, inakutana na KMC yenye hasira za kufungashiwa virago na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Sven amesema kuwa amekiandaa kikosi chake kwa utulivu ili kuona kinashinda mbele ya KMC ili kupata pointi tatu muhimu.
“Tumetoka kushinda mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho mbele ya Stand United, macho yetu kwa sasa ni kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya KMC, imani yangu tutapata matokeo chanya yatakayotupa pointi tatu” amesema.
Post a Comment