HARERIMANA Haruna, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kwa sasa anahofia kibarua chake kuota nyasi kutokana na mwenendo wa timu yake ulivyo ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na kupigwa chini kwenye Kombe la Shirikisho.

KMC ilitolewa na Kagera Sugar kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penalti 2-0 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu.

Kwenye Ligi Kuu Bara KMC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 24.

"Wachezaji wamekuwa hawanielewi kile ambacho ninawaambia kipindi cha kwanza wanafanya vitu vya kitofauti wanavyovijua wao jambo linalonifanya kipindi cha mapumziko nianze kuwaelekeza upya, nina mashaka huenda mambo yatakuwa magumu ndani ya KMC hasa kwa upande wa nafasi yangu," amesema.

Harerimana alitua KMC akitokea timu ya Lipuli FC ambapo alidai kuwa hakulipwa stahiki zake kwa muda mrefu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.