UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa baada ya kumalizana na Ihefu sasa akili zao ni kwenye mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tazania.

Azam FC ilipenya kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho na kutinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 mbele ya Ihefu ya Mbeya kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Februari 26.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa mipango inakwenda sawa na wanajipanga kuona wanapata pointi tatu mbele ya JKT Tanzania.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 45 baada ya kucheza mechi 24.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.