FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Alliance FC amesema kuwa ushindi wao walioupata mbele ya JKT Tanzania sio ujanja bali ni bahati kwani penalti hazina mwenyewe.

Minziro alikiongza kikosi chake kwenye ushindi wa panalti 5-3 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Shirikisho.

Dakika tisini zilikamilika kwa timu hizo kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.

Minziro amesema:"Haikuwa kazi nyepesi na wala sio ujanja wangu kwani wapinzani wetu walipambana na mwisho wa siku penalti hazina mwenyewe nasi tumepita.

"Tutakwenda kupambana hatua inayofuata kwani tunatambua kwamba ushindani mbele ni mkubwa kuliko wakati wa sasa," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.