MWEZI Februari, mabingwa watetezi Simba wamecheza mechi saba za Ligi Kuu Bara na wameambulaia kichapo mechi moja mbele ya JKT Tanzania.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Uhuru, Februari 7 na bao pekee la ushindi lilifungwa na Adam Adam kwa kichwa mbee ya beki kisiki Pascal Wawa.
Simba ilikuwa inasaka pointi 21 imeambulia pointi 18 na tatu zimeyeyuka jumlajumla.
Kwa upande wa mabao ya kufunga, Simba imefunga mabao 12 huku ikikubali kufungwa mabaoa matatu.
Simba 2-0 Coastal Union, Februari 1, Simba 2-1 Polisi Tanzania, Simba 0-1 JKT Tanzania, Februari 7, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Februari 11, Lipuli 0-1 Simba , Februari 15, Simba 1-0 Kagera Sugar, Februari 18, Simba 3-1 Biashara United, Februari 22.
John Bocco nahdha wao amekuwa kinara kwa mwezi Februari, ametupia mabao matatu na ametoa pasi moja ya bao.
Post a Comment