JERRY Muro aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga, amesema kuwa kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ni bora kuliko kocha Mkuu wa sasa wa Yanga Luc Eymael raia wa Ubelgiji.
Muro amesema kuwa huo ni mtazamo wake na haina maana kwamba hathamini mchango wa Eymael.
"Maoni yangu na mtazamo wangu ni kwamba, Mkwasa ni bora kwani amekuwa na timu wakati mgumu na anapata matokeo mazuri ila haimaanishi kwamba namchukia Mzungu hapana kwangu mimi tu na haya ni maoni yangu," amesema.
Post a Comment