MACHI Mosi, Mbwana Samatta atakuwa na kazi ya kuiongoza timu yake ya Astn Villa kwenye mchezo wa Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kulitazam kwa jicho la pekee taji hilo la Carabao na utapigwa Uwanja wa Wembeley.
Huo utakuwa mchezo wa tano kwa Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Kutokana na uzito wa mchezo huo baba mzazi wa Mbwana Samatta, Ally Samatta naye amekwea pia leo ili kwenda kumcheki mwanae akiwa uwanjani akipambana.
Post a Comment