IMEELEZWA kuwa nyota wa timu ya Yanga, Bernard Morrison ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu hiyo inayopambana kutwaa taji la Ligi Kuu Bara lililo mikononi mwa Simba.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye mabao mawili ndani ya Bongo na pasi tatu za mabao ilielezwa kuwa alikuwa kwenye hesabu za Simba ili wamtumie kwenye michuano ya kimataifa pamoja na timu nyingine mbili kutoka Afrika Kusini.
Habari zinaeleza kuwa mabosi wa Kampuni ya GSM wameamua kumalizana naye kwa kukaa naye chini na kumpa mkataba huo.
"Awali mkataba wake ulikuwa ni wa muda wa miezi sita ulikuwa unampa uhuru kuzungumza na timu nyingine na watani kama kawaida jicho lao limewashtua, ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja na nusu.
"Kwa sasa presha imeshuka na kazi itafanyika bila mashaka kwani ana mkataba wa miaka miwili kwa sasa ndani ya Yanga," ilieleza taarifa hiyo.
Post a Comment