Mkuu waWilaya ya Arumeru, Jerry Murro, leo amerejea klabuni Yanga na kuzungumza mambo kadhaa akiwapa wanachama matumaini kuwa yeye na wengine ambao hauwataja, wamerejea.

Baadhi ya kauli alizotoa, hizi hapa:


“Nimekuja nimeagizwa, kawaambie machozi yao sasa mwisho, hakuna mtu tena atalia ndani ya Yanga.

“Tunacheza na Gwambina, kesho ndio tunaanza, wachezaji watacheza ndani na sisi tutacheza nje. Tutaulinda uwanja na tutapambana na anayetaka kuionea Yanga.

“Tumezungumza na wachezaji, tutahakikisha wanapambana kufa na kupona, wachezaji wako tayari na sasa hatutaki ushindi wa bao moja bila.

“Potelea mbali, liwalo na liwe na tunataka kuanzia kesho watu wajue na wazikie kuna watu wamekerwa. Nawatangazia wananchi wenye timu yao, wale wengine ni mabwanyenye, msikate tamaa njooni uwanjani.

“Wachezaji wamelipwa, wananuka fedha na familia zao zijue na sasa wananuka fedha.

“Tumeimarisha ulinzi kambini, sasa tunapekua mitandao yao ya simu. Kama kuna wale wanaotuhujumu, tutawataja uwe Simba, uwe bodi ya uwe TFF.

“Ukichukua na wanachama wa Yanga undue umechukiwa na Mungu. Tunajua watu wamewekwa kutuhujumu mchana na usiku.

“Kama wewe wa mike, matopeni au mchangani utatukuta usiku, tunalinda timu yetu na nembo.

“Kumbukeni baada ya Magufuli ujue kinachofuata ni Yanga.

“Kumbukeni Yanga ilimpigania Haji wakati anaumwa macho. Mwacheni Nugaz aipiganie Yanga.

“Namuambia mmiliki wa Gwamibina awe makini, asikae karibu na Simba, atatupa hasira yutampiga nane.

“Sijarudi Yanga kama msemaji, nimekuja kama mwanachama na kiongozi mstaafu ninayeguswa. Password tulikuwa nayo sisi, nimerudi nayo pia

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.