BEKI wa Simba, Yusuph Mlipili amesema kuwa bado yupo ndani ya kikosi cha Simba wakati ukifika ataonekana uwanjani.
Mlipili hajawa na msimu mzuri ndani ya msimu wa 2019/20 kwa kushindwa kucheza ndani ya kikosi cha kwanza zaidi ya kuishia benchi kutokana na ushindani wa namba ndani ya kikosi hicho.
Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa nyota ambao wanaweza kusepa ndani ya kikosi cha Simba ni pamoja na beki huyo kutokana na kubakiza kandarasi ya miezi sita.
Mlipili amesema:"Nipo ndani ya Simba na ninajua kwamba mashabiki wanapenda kuniona wakati ukifika nitaonekana na nitafanya kazi, kila kitu kinawezekana,".
Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa Mlipili ni mchezaji wa Simba
Post a Comment