UONGOZI wa Mtibwa Sugar umewaomba mashabiki kuendelea kuipa sapoti timu hiyo licha ya kupitia kipindi cha mpito kwa sasa.

Februari, Mtibwa imecheza mechi saba haijafunga bao kwenye mechi zote hizo zaidi ya kuambulia sare moja na kupoteza sita. Mchezo wake wa mwisho ilifungwa bao 1-0 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine.

Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kufungwa haimaanishi ndio mwisho wa mahesabu bado kuna kazi inaendelea kufanyika.

"Ninawaomba mashabiki waendelee kuipa sapoti timu kwani kwa sasa inapitia kipindi cha mpito, kufungwa haina maana kwamba usiendelee kupambana hapana kazi lazima iendelee," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.