Kinda wa zamani wa Arsenal Tyrell Robinson ,22, ameingia kwenye headlines nchini England baada ya Polisi kumshitaki kwa kushiriki mapenzi na mtoto (ngono), Tyrell Robinson baada ya kukutwa na tuhuma hiyo nzito club yake ya Bradford City ya League Two England imemfukuza rasmi.
Baada ya uchunguzi Robinson amekutwa na kesi ya kujibu na atalazimika kuwepo Mahakamani April 7 2020, club imemuondoa na kusema kuwa kwa sasa haitakuwa ikitoa kauli yoyote kuhusiana na kesi au mchezaji huyo kutokana na sasa kutokuwa chini yao tena wameachana nae.
Tyrell Robinson alizaliwa September 16 1997 Basildon England na baadae kuanza soka lake la vijana katika club ya Arsenal hadi 2017 akiwa na umri wa miaka 19 alipojiunga na club ya Bradford City ambayo leo imeamua kumwaga rasmi kutokana na kosa hilo alilolitenda toka 2018 August.
Post a Comment