Na Saleh Ally
KOCHA
Dean Smith wa Aston Villa, aliamua kufanya mabadiliko ya mapema katika
dakika ya 58 katika mechi dhidi ya Bournemouth wakiwa nyuma kwa mabao
2-0.
Alimtoa
Anwar El Ghazi raia wa Uholanzi na nafasi yake ikachukuliwa na
Mwingereza, Keinan Davies ambaye kama unakumbuka katika mechi ya Carabao
dhidi ya Leicester City, aliingia kuchukua nafasi ya Mtanzania, Mbwana
Samatta.
Mabadiliko
hayo yalikuwa msaada mkubwa kwa Villa ambao walipata bao likifungwa na
Samatta baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na beki wa Bournemouth. Hili
bao limeifanya Tanzania kuwa nchi ya 99 raia wake kufunga bao katika
EPL.
Pamoja
na kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1, takwimu zinaonyesha Villa
walitawala kila idara na kiungo wake mchezeshaji, Jack Grealish ndiye
alikuwa mchezaji bora wa mechi. Lakini Watanzania wanalia naye kila
upande kwamba alikuwa akimnyima pasi Samatta.
Grealish
ni mchezaji tegemeo zaidi ya Samatta na amekuwa msaada mkubwa katika
kikosi hicho na kamwe hajawahi kulalamikiwa kwa uchoyo kwa kuwa takwimu
ndio uhalisia. Lakini Kibongobongo, watu wanalia hadi katika mitandao ya
Klabu ya Aston Villa ambalo si jambo zuri.
Unaposema
mchezaji mchoyo ni yule asiyefikisha pasi kwa wenzake. Pasi nazo zina
aina nyingi, inawezekana zile kwa ajili ya kuchezesha timu, kulinda au
kusaidia kutengeneza bao kwa maana ya asisti.
Katika
takwimu za Ligi Kuu England, Grealish wao wanamuita “Mtoto wa
nyumbani”, anaongoza kwa mabao akiwa amefunga saba akifuatiwa na Wesles
mwenye matano halafu Anwar El Ghazi aliyefunga manne.
Upande
wa pasi za mwisho, yaani asisti, Grealish anaongoza akiwa na tano,
akifuatiwa na El Ghazi mwenye nne halafu Frederic Gulbert aliyetoa
mbili. Maana yake si kweli kuwa hataki wenzake wafunge kwa kuwa yeye
ndiye aliyetoa pasi nyingi zilizozaa mabao ya timu hiyo katika msimu huu
wa EPL.
Kwenye
pasi ambazo zimefika, Grealish anaongoza tena akiwa na 800, akifuatiwa
na beki Tyrone Mings mwenye 747 na Douglas Luiz aliyepiga 572. Kama
ndiye aliyetoa pasi nyingi zaidi ya wengine, vipi tuamini kuwa hataki
kutoa pasi au anamnyima Samatta? Ni fikra potofu ambazo wengine
tumezibeba kwa hisia za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kama
angekuwa mchoyo wa pasi, basi asingekuwa na asisti nyingi, sasa
anaongoza. Kama angekuwa hatoi asisti, bado asingekuwa mchoyo kwa kuwa
kapiga pasi nyingi zilizofika kuliko mchezaji yeyote wa Villa.
Mfano
mzuri wa pasi zilizofika ni ile maridadi aliyompa Samatta katika mechi
ya Carabao Cup dhidi ya Leicester ambao sote tulikiri kuwa Samatta
hakutulia, akaipoteza.
Hakuna
hata mmoja amesikika akisifia ile pasi maridadi aliyopewa na Grealish
ambayo inakuwa kati ya pasi 800 zilizofika za kiungo huyo. Kama Samatta
angefunga, basi leo Grealish angekuwa na pasi 799 na asisti 8. Lakini
bahati mbaya Samatta hakuwa ametulia na inawezekana utofauti wa soka la
England akiwa mgeni kwa mara ya kwanza.
Ukiachana
na hivyo, bao la Samatta la kwanza katika mechi ya kwanza ambalo
limetengeneza faraja kwa Watanzania, lilianzia kwa Grealish baada ya
kupokea pasi ndefu, akawalaghai mabeki wa Bournemouth na kupiga pasi
safi ya chini iliyofika kwa Davies ambaye aligeuka na kupiga shuti kali
lililozuiwa na mpira ukamfikia Samatta, akafanya yake.
Hakuna
ubishi kadiri wanavyokwenda wanazoeana, kila mmoja atajua mwenzake
anachezaje na kuanza kupeana pasi zaidi kwa kuwa mikimbio ndio namna ya
kujua mchezaji mwenzako anacheza vipi.
Pamoja
na hivyo, kila wanavyozidi kucheza, itakuwa rahisi wa Kocha Smith
kuendelea kuwapa mipango na kupanga njia za kumfikishia mipira mingi
Samatta kwa njia rahisi zaidi au inayowahadaa zaidi wapinzani.
Si
kweli Grealish anaweza kumnyima mipira Samatta, hasa akijua wazi wako
katika wakati mgumu na kunahitajika mtu wa kumalizia kazi zake nzuri.
Kwa
wenzetu takwimu bora si mabao pekee, asisti zinakuza soko la mchezaji,
pasi zilizofika zinaongeza bei yake. Hivyo Grealish kama play maker,
anazihitaji na angependa kuona mabao mengi yanatokana na pasi zake nzuri
zaidi.
Bila
shaka, msimu ujao wa Premier League atakuwa mmoja wa wachezaji
watakaotakiwa na klabu kadhaa kutokana na ubora anaouonyesha, hivyo
tusianze kuwaza Ki-Ligi Kuu Tanzania Bara, hali ya wengi kuona kulaumu
ndio kuuzungumzia mpira.
Kama
una takwimu zinazoonyesha Grealish alimnyima Samatta pasi ngapi,
onyesha kama huna achana na mawazo hayo potofu na kataa kuwa bendera
fuata upepo na ikiwezekana sasa tuendane na Samatta, tuwe na mawazo ya
Ki-Premier League.
Mwisho
nikukumbushe, kadiri Samatta na Grealish wanavyozidi kuzoeana katika
chemistry ya uchezaji, mabao mengi ya Samatta yatatokea kwa kiungo huyo
mchezeshaji hatari na matata kabisa.
Post a Comment