Juventus wanajiandaa kuwapa Manchester United wachezaji watatu ili kubadilishana na kiungo Paul Pogba. (Mirror)
Mpango huo kama utafaulu, utawahusisha wachezaji Danilo, 28, na Joao Cancelo, 25. (Goal.com)
Arsenal wanaweza kuelekeza nguvu zao zote katika kumsajili beki wa kati wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 20, kama mbadala wa beki wa JuventusDaniele Rugani - lakini Leipzig wanataka pauni milioni 50 ili kumuachia beki huyo. (Mirror)
Everton wamekusanya 'kapu' la usajili lenye thamani ya pauni milioni 100 kumsajili msahambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26. Ofa hiyo inahusisha pia Everton kuwapa Palace mshambuliajii Cenk Tosun na kiungo James McCarthy, wote wana miaka 28. (Sun)
Zaha ambaye ni raia wa Ivory Coast anatarajiwa kujiunga na Everton kabla ya Alhamisi ambapo diisha la usajili Uingereza linafungwa, Palace wapo tayari kupokea kitita cha kufikia pauni milioni 65. (Independent)
Leicester haitamsajili Nathan Ake katika dirisha hili la usajili baada ya klabu ya Bournemouth kutaka dau la pauni milioni 75 kwa beki huyo raia wa Uholanzai. (Sky Sports)
Arsenal wamejaribu kufikia makubaliano na nahodha wao Laurent Koscielny - lakini beki huyo mwenye miaka 33, ambaye aligoma kusafiri na timu kwenda Marekani, pia amegoma kufanya mazungumzo na klabu. (Mirror)
Manchester United wataendelea kupokea ofa kwa ajili ya mshambuliaji wao Romelu Lukaku, 26, lakini yawezekana wasitafute mbada wake endapo ataondoka baada ya kuchipukia kwa kinda Mason Greenwood, 17. (ESPN)
Lukaku ana uwezekano mkubwa wa kujiunga Inter Milan kuliko Juventushususani endapo Man United itashindwa kumpata Paulo Dybala, 25. (Express)
Manchester United wanakaribia kumsajili kiungo wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, baada ya kiungo wa Sporting Lisbon Mreno Bruno Fernandes - ambaye alikuwa anawindwa na Man United kuweka wazi nia yake ya kujiunga na Spurs. (AS)
Tottenham inajiandaa kupokea ofa za kiuhalisia kutoka klabu za Ulaya kwa ajili ya Eriksen endapo mchezaji huyo hatauzwa ndani ya Uingereza mpaka dirisha litakapofungwa nchni humo kesho Alhamisi. (Telegraph)
Post a Comment