WACHEZAJI wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England wameunda umoja wao ambao una malengo ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kupambana na Virusi vya Corona.
Muasisi wa umoja huo ni nahodha wa Klabu ya Liverpool Jordan Henderson ambaye ameungwa mkono na mmakapteni wenzake ikiwa ni pamoja na Harry Maguire wa Manchester United.
Kwa sasa Ligi Kuu England imesimamishwa na inatarajiwa kurejea pale hali itakapokuwa shwari kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao ni janga la dunia kwa sasa.
Mfuko huo ambao unawajumuisha wachezaji wote wanaoshiriki Ligi Kuu England umepewa jina la Players Together ambapo watashirikiana na Shirika la NHS kwa upande wa misaada pamoja na NHSCT.
Taarifa juu ya uwepo wa kundi hilo ilitolewa jana Jumatano ambapo wachezaji wamewapa majukumu manahodha wa timu zote kusimamia masuala ya makusanyo ya fedha ili kuongeza nguvu kwenye sapoti ya kupambana dhidi ya Corona.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.