UONGOZI wa Simba umesema kuwa hatma ya wachezaji wote ndani ya kikosi hicho ni pale ambapo Ligi Kuu Bara itakamilika ndipo watataja wale watakaochwa na watakaoongezewa mikataba.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona kuna wachezaji ambao maisha yao kikosi cha kwanza yalikuwa magumu.

Nyota hao ni pamoja na Shiza Kichuya, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Yusuph Mlipili.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza amesema kuwa kwa sasa itakuwa ngumu kuwataja wachezaji watakaochwa na watakaobaki ndani ya Simba.

"Bado ligi haijaisha licha ya kwamba kwa sasa imesimama, haitapendeza iwapo watatajwa wale watakaoachwa kwa muda huu itawaumiza hivyo acha maisha yaendelee," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.