BEKI wa Barcelona, Sergi Roberto amefunguka kuwa anatamani kuona kuwa kama La Liga itarejea basi klabu zipewe muda mfupi kidogo wa mazoezi kwa kujipanga kisha kuendelea.
Ligi kwa sasa zimesimama ikiwemo La Liga kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa COVID19 wa Virusi vya Corona ambao unasambaa kwa kasi ndani ya Hispania na kwingineko duniani.
Roberto alisema:” Matumaini yetu ni kuona kuwa kabla ya La Liga kurejea basi timu zinapata nafasi ya kufanya mazoezi kwa pamoja japo kwa sasa kila mtu anafanya kivyake kutokana na hali halisi,”alisema beki huyo.
Post a Comment