MCHEZAJI wa PSG, Mauro Icard amesema ameamua kutimka Ufaransa na familia yake kurejea Italia na kujitenga kwa kuhakikisha wanaepuka Virusi vya Corona.
Icard kwa sasa anacheza PSG kwa mkopo akitokea katika klabu ya Inter Milan ya nchini Italia ambako ndiko familia yake ila ni raia wa Argentina.
Nyota huyo amesema: “Nimeamua kurudi nyumbani na hapo tumeruhusiwa na kupewa tahadhari na Serikali kwa kuhakikisha tunajilinda ili kuwa salama.
“Nimerejea huku sababu ndipo familia ilipo pamoja na mke wangu hivyo tutaendelea kujitenga wenyewe mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa.
“Nitakuwa hapa na familia yangu ninaamini hili janga litapita na tutarudi katika maisha yetu ya kawaida sababu hali siyo nzuri," amesema.
Post a Comment