RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema msimu ujao klabu hiyo itafanya usajili bora ambao hautategemewa.
Kuelekea msimu ujao Klabu ya Barcelona imekuwa ikihusishwa kusajili nyota wengi wakali huku ikielezwa kuwa na mpango wa kumrejesha Neymar Jr ndani ya Barcelona.
Akizungumza na Mundo Deportivo, rais alisema: “Kwa sasa siwezi kusema ni nani ambaye tutamsajili msimu ujao, ila tunahitaji kuwa na wachezaji bora.
Kiongozi huyo alisema licha ya uwepo wa Virusi vya Corona bado mipango yao ipo palepale kwenye usajili wao.
“Mipango yetu bado, Abidal na wenzake wanaendelea kupambana japo najua msimu utakuwa mgumu kwa upande wa fedha kutokana na uchumi kuyumba.
Hata hivyo, ripoti kutoka nchini Hispania zinaeleza kuwa Barcelona imekuwa ikipambana katika kuwanasa Neymar na Lautaro.
Imeelezwa kuwa Barcelona kitendo cha kutaka kumrejesha Neymar basi itawagharimu kiasi cha euro milioni 180, Huku Barca inataka kulipa kiasi cha euro milioni 70 kumnasa Lautora pamoja na Arturo Vidal.
Barcelona kwa sasa inapambana kuhakikisha ina imarisha safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inamtegemea Messi kwani Suarez na Dembele wametupwa nje kutokana na majeruhi.
Post a Comment