ALBERTO Yaque, wakala wa Lautaro Martinez anayekipiga Inter Milan amesema hajafuatwa na klabu yoyote kwa sasa na wala mchezaji wake hajauliza habari za kutimka ndani ya timu yake kwa sasa.
Nyota huyo amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu tofauti hasa Barca na Madrid zimekuwa zikitajwa kuiwinda saini yake.
Yaque alisema: “Kwa sasa hakuna timu ambayo imeongea na mimi wale wafanya kazi wao kwa hiyo tunaendelea na mambo mengine.
“Imekuwa ikiripotiwa katika vyombo vya habari kuwa Madrid na Barca ndiyo wanamuhitaji, lakini mwenye hata hajawahi kusema kitu cha namna hiyo na hata hajawahi kuniuliza kuhusu hizo tetesi.
Kwa msimu huu, Martinez amekuwa katika kiwango cha juu na hata kombinesheni yake na Lukaku imeonekana kuzaa matunda ndani ya kikosi cha Inter Milan
Post a Comment