UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wachezaji wao wote wamekuwa wakionyesha juhudi za kufanya mazoezi wakati huu wa mapumziko jambo ambalo linapaswa liwe na mwendelezo muda wote.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo inaelezwa na wataalamu kwamba vinasambaa kwa njia ya hewa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya wachezaji kwa ukaribu jambo ambalo linaleta matumaini kuwaona kila mmoja akitimiza kile alichopangiwa.

"Kocha mkuu Luc Eymael alitoa program kwa wachezaji na kila mmoja inaonyesha kuwa anafanya kile ambacho ameambiwa jambo ambalo linamaanisha kwamba tukirudi tutakuwa vizuri.

"Kikubwa kwa sasa ni kuona kwamba hali inarejea kama zamani na tunakuwa salama kwani Virusi vya Corona vinatufanya tunakosa mengi, mashabiki pia wakiwa nyumbani ni muhimu kuchukua tahadhari," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.