BEKI kisiki wa Simba, Pascal Wawa, amesema kuwa Virusi vya Corona siyo vya kuchukulia utani, ni lazima kila mmoja achukue tahadhari.
Wawa amesema kuwa kwa sasa anafanyia mazoezi ndani kutokana na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.
“Nipo nyumbani na hali bado haijawa nzuri kwa sasa tunaomba Mungu mambo yarudi kama zamani kwani kwa sasa ninafanyia mazoezi nyumbani, hivyo ni lazima tuchukue tahadhari kuhusu Corona,” amesema Wawa.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilitoa tamko hilo Machi 17.
Post a Comment