BEKI  wa Real Madrid, Jesus Vallejo anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Granada amefunguka kuwa huenda akaendelea kusalia katika klabu hiyo kwa msimu ujao.

 Vallejo anaweza kusalia moja  kwa moja katika Klabu ya Granada, huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika Juni 30, mwaka huu na hapo ndipo atachagua.

Beki  huyo alikosa namba ndani ya Madrid baadaye aliamua kuangalia ustaarabu mwingine ili kuendeleza kipaji chake.

Vallejo alisema: “ Ninafuraha kwani  wameniambia  kuwa wanataka niendelee kuwa  hapa japo nipo kwa mkopo.
“ Binafsi  ni furaha  kuendelea kuwa hapa Granada hii inaonyesha kuwa wameona kuna kitu ndani yangu ndiyo maana wanahitaji nifanye hivyo na si vinginevyo.

“Kwa sasa naendelea kujijenga  ili kuwa bora,sababu haifahamiki ligi itarudi lini, lakini nahitaji kuwa tayari wakati wowote ule,” alisema Vallejo.

 Beki huyo awali alitolewa kwa mkopo kwenda England katika klabu ya Woves, lakini mambo hayakwenda vizuri.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.