KOCHA wa zamani wa Atletico Madrid ya Vijana, Milinko Pantic amefunguka kuwa ndoto yake nikuja kuifundisha timu ya klabu hiyo hapo mbeleni.

 Mserbia huyo kwa sasa hana timu, anasema ndoto yake ni siku moja kuja kukinoa kikosi cha Atletico Madrid.

 Kwa sasa Klabu ya Atletico Madrid inanolewa na staa wake wa zamani Diego Simeone ambaye  ameifanya timu hiyo kuwa bora.

 Mpaka sasa ligi zimesimama tayari Simeone alikuwa ameipeleka timu hiyo robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 Miaka  ya 1995/98  kocha huyo aliwahi kuichezea klabu kama kiungo na alicheza kwa mafanikio na baadaye alikuja kubahatika  kuifundisha timu ya vijana ya klabu hiyo.

 Milinko  alisema:“Ndoto yangu kubwa ni kuja kuifundisha Atletico Madrid ndiyo kitu muhimu kwangu na nitafurahi sana kama hili litatimia siku moja.

“Naamini ipo siku huo muda utafika tu na hii ndoto itakamilika, kwa hilo nipo tayari wakati wowote ingawa sijui itakuwa lini na mwaka gani kikubwa ni kutimiza kile ambacho nakitaka,”alisema Milinko.

 Ikumbuke kuwa Milinko walicheza pamoja katika kikosi cha Atletico Madrid kipindi cha nyuma wakati wanacheza soka.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.