INAELEZWA kuwa dau la nyota wa Coastal Union, Bakari Nondo ni zaidi ya milion 90 kutokana na uwezo wake alionao ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa.

Nondo amekuwa akihusishwa kutua ndani ya Simba ambao inaelezwa kuwa dau lao ni milioni 85 zilizowekwa mezani.

Nyota huyo ambaye pia ni nahodha wa Coastal Union amekiongoza kikosi chake kwenye mechi 28 na kimefungwa mabao 19 kikiwa ni cha pili msimu huu kufungwa mabao machache ndani ya ligi huku nafasi ya kwanza ikiwa ni kwa Simba ambao wamefungwa mabao 15 kwenye mechi 28 za ligi.

Meneja wa nyota huyo, Mussa Kassa amesema kuwa hawezi kutaja dau la mchezaji wake kwani anaamini kuwa uwezo wake ndio utakaompa thamani uwanjani.

"Ni mchezaji mzuri kazi yake inaonekana ila dau lake siwezi kuliweka hadharani ni makubaliano na timu ambayo inamhitaji," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.