RIPOTI ya Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael iliyotoa mezani inaelezwa kuwa anahitaji nyota wawili wazawa ambao watajiunga na Yanga msimu ujao ili kuongeza makali ya sau ya ushambuliaji.
Kwa sasa wakati Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa na Serikali kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, safu ya ushambuliaji ya Yanga ilikuwa imetupia mabao 31 baada ya kucheza mechi 27.
Habari zinaeleza kuwa Eymael ameamua kuacha majina mengi ili kuwapoteza maboya wapinzani wao Simba ambao wamekuwa wakiinglia kati madili yao na kusepa na wachezaji wao.
"Eymael kwa sasa bado hajarejea Bongo kwa kuwa mipaka imefungwa kwao Ubelgiji ila kabla ya kuondoka aliacha majina ya wachezaji wazawa hasa kwa nafasi ya ushambuliaji.
"Majina hayo ni mengi yakiwa na lengo la kuwachanganya wapinzani wa Yanga ila tayari mipango ipo sawa na atakaporejea kazi itaanza ya kuwafuatilia tena," ilieleza taarifa hiyo.
Majina hayo inatajwa kuwa ni Reliants Lusajo nahodha wa Namungo FC, Paul Nonga nahodha wa Lipuli FC hawa wote wametupia mabao 11, Daruesh Saliboko nyota anayekipiga Lipuli ametupia mabao nane, Yusuph Mhilu nyota anayekipiga ndani ya Kagera Sugar ametupia mabao 11 Marcel Kaheza mshambuliaji anayekipiga ndani ya Polisi Tanzania ametupia mabao saba na pasi tano za mabao.
Kuhusu suala hilo Lusajo amesema:"Ni kweli kuna jambo ambalo lipo na Yanga lakini mimi bado nipo Namungo ambayo ni timu yangu ofa yao ninaipa kipaumbele.
Mhilu amesema:"Awali nilikuwa ninafuatwa na watu wa Yanga ambao walikuwa wananiambia ninatakiwa nirudi lakini kwa sasa bado haijawa hivyo,".
Nonga amesema:"Bado nina mkataba na Lipuli ila ikiwa kutakuwa na dili kubwa zaidi ni suala la kukaa mezani,'.

Post a Comment