UONGOZI wa Simba umesema kuwa miongoni mwa sababu kubwa zinazowafanya wailinde saini ya nyota wao Clatous Chama ni pamoja na kuthamini mchango wake alioufanya ndani ya Klabu ya Simba.

Chama amewaweka kwenye mvutano mkubwa Simba na watani zao wa jadi Yanga kutokana na kile ambacho Yanga walieleza kuwa walikuwa na mazungumzo naye ili kuipata saini yake.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa miongoni mwa kazi ambayo Chama ameifanya ni pamoja na kuifikisha Simba hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 "2018 bao lake la kisigino lipo kwenye kumbukumbu tena aliwafunga ndugu zake wa Zambia likatupeleka kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hapo akitokea mtu akaleta utani juu yake ni lazima twende naye sawa.

"Tunatambua umuhimu na kanuni za usajili hivyo ni lazima kila kitu kifuate ule weledi na kuzingatia kanuni kwani mambo yapo wazi, Chama ni mchezaji wetu na ana mkataba mrefu ndani ya Simba.

"Zile presha ambazo tuliwapa kupitia kwa mchezaji wao Papy Tshishimbi wasifikirie kuzileta kwetu kupitia Chama, hilo haliwezekani," amesema.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa suala la Chama wao walichukulia ni sehemu ya utani hivyo wanawaomba radhi mashabiki wa Simba na uongozi kiujumla.

Ishu ya Chama kwa sasa imetinga Shirikisho la Soka la Mpira Tanzania (TFF) ambapo Simba imepeleka malalamiko kwa kueleza kuwa Yanga imeelezwa kuwa imefanya mazungumzo na mchezaji wao Chama ilihali ana mkataba kwa sasa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.