MAKAMU Mwenyekiti wa Klabu ya Alliance, Stephano Nyaitati amefunguka kuwa uongozi wa klabu hiyo umekuwa hauingilii majukumu ya makocha kama inavyodaiwa.
Hii inakuja kutokana na ile tabia ya kufukuza makocha kila wakati na hivi karibuni waliokuwa makocha wa timu hiyo, Felix Minziro na msaidizi wake Wandiba alidai kuingiliwa katika majukumu yake.
Nyaitati amesema:“Kuna taarifa kwamba uongozi wa Alliance chini ya Mkurugenzi wake James Bwire zinadai tumekuwa tukiwaingilia makocha kwenye majukumu yao ukweli ni kwamba sisi huwa hatufanyi hivyo ndiyo maana tumekuwa tukileta wataalamu na yanapotokea mabadiliko yanakuwa ya kawaida sana hivyo isitafsiriwe vibaya"
"Makocha wengi wakipigwa chini kutokana na uwezo wao mdogo ama sababu nyingine wamekuwa wakisema mkurugenzi wetu anaingilia katika majukumu yao naomba ieleweke kwamba hatuwaingili kwenye majukumu yao bali tumekuwa tukifanya mabadiliko ya kawaida ambayo kimsingi huweza kufanywa na klabu yoyote,”amesema Nyaitati.
Kwa msimu huu tu, Alliance imewatimua Athuman Bilali, Habib Kondo, Malale Hamsini na, Fred Felix Minziro.
Chanzo: SpotiXtra
Post a Comment