MOHAMED Rashid, nyota wa JKT Tanzania anayekipiga kwa mkopo akitokea Simba amesema kuwa kuna umuhimu wa kila mmoja kuchukua tahadhari ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona ili kubaki salama.

Akizungumza na Saleh Jembe, Rashid amesema kuwa amekuwa akitumia muda mwingi nyumbani kutokana na kushindwa kuendelea na mazoezi ikiwa ni njia ya kujilinda na Corona.

"Muda mwingi natumia nikiwa nyumbani kwa sasa tofauti na wakati ule kabla ya janga hili kutokea, nimekuwa nikiwasihi na wengine pia kama hawana shughuli ya muhimu itakayowatoa nje wabaki nyumbani.

"Kuna vitu vingi tunakosa kwa sasa lakini hakuna namna ni lazima tuombe hili janga lipite na kila mmoja achukue tahadhari," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.