WAZIR Jr, mshambuliaji wa Mbao FC amesema kuwa anaimani kuwa timu yao haitashuka daraja kutokana na mipango ambayo itapangwa baada ya ligi kurejea.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wazir amesema kuwa mipango mikubwa ni kuona timu inapata matokeo chanya kwenye mechi zilizobaki jambo litakalowabakiza kwenye ligi.
"Bado tuna nafasi ya kubaki ndani ya ligi kutokana na mipango ambayo tutakuja nayo pindi ligi itakaporejea, imani yangu tutakuwa vizuri na tutapambana kupata matokeo," amesema.
Mbao FC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 28
Post a Comment