UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hautakubali kumruhusu mchezaji wao yeyote kusepa iwapo Kocha Mkuu, Luc Eymael atahitaji saini yake ikiwa ni pamoja na Papy Tshishimbi.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba na Tshishimbi ambaye inaelezwa kuwa Simba wapo kwenye mpango wa kuinasa saini yake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana mpango wa kubaki na wachezaji wote wanaohitajika na Kocha Mkuu Eymael.

"Mpango mkubwa ni kuona kwamba wale ambao wanahitajika na Kocha Mkuu wanabaki kwani uwezo upo na nia tunayo kikubwa ni kuwa na subira tu.

"Kuhusu Tshishimbi bado tunaendelea kuzungumza naye wakati utazungumza kwani tunatambua mchango wake ndani ya Yanga na umuhimu wake pia," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.