SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa kwa kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona wachezaji ambao hawatafuata program walizopewa watarudisha nyuma maendeleo ya timu.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa ni jambo la msingi kwa wachezaji wote kuzingatia program ambazo wamepewa na makocha wao ili kulinda vipaji vyao pamoja na kutoziangusha timu zao.
“Wachezaji ambao watashindwa kufuata program ambazo wamepewa na makocha itakuwa ni kurudisha nyuma maendeleo ya timu kiujumla kwani wao ndio wanacheza kutafuta matokeo wasipofanya mazoezi hawatakuwa bora.
“Iwapo ligi itarejea na wao hawajafanya mazoezi itakuwa kazi nyingine kwa makocha kuanza kufundisha upya huku mechi zikiwa zimebaki chache ndani na ikumbukwe kuwa nyingine zipo kwenye hatari ya kushuka daraja,” amesema Matola.
Post a Comment