JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wameshauriwa kuacha kula vyakula vyenye mafuta mengi ili kuepuka kuongezeka uzito ghafla.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa kila mchezaji amepewa program yake ya kuifanya na ushauri wa kufuata akiwa nyumbani.

"Kuna program ambayo tumepewa na kila mchezaji anafuata kazi yake ila tumeshauriwa kuacha kula vyakula vyenye mafuta ikiwa ni pamoja na Chips kuku ili kuzuia kuongezeka uzito ghafla.

"Pia hata kula mara kwa mara wali pia tumeambiwa tuangalie, hivyo mimi binafsi ninapenda kujali ratiba za msosi na aina ya vyakula ambavyo ninakula," amesema.

Abdul kabla ya ligi kusimama alikuwa ni kinara wa mipira ya mwisho akiwa ametoa pasi tano za mabao huku Yanga ikiwa imefunga mabao 31.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.