MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba amesema kuwa sababu kubwa inayomfnya afunge akiwa ndani ya uwanja ni umakini wa kutumia nafasi anazozipata pamoja na ushirikiano wa wachezaji wenzake.

Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, Kagere alikuwa ametupia mabao 19 na pasi tano huku Simba ikiwa imefunga mabao 63.

Kagere amesema,:-" Ni ngumu kufikia mafanikio bila kuwa na ushirikiano na wachezaji wengine lakini ushirikiano unatufanya tunakuwa pamoja hicho kinanipa nguvu ya kufunga nikiwa uwanjani.

"Nafasi yangu ni mshambuliaji nikipata nafasi ninaitumia pia nikishindwa basi nitatengeneza kwa ajili ya wengine,".

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 71

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.