MRISHO Ngassa, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa sasa amejichimbia Mwanza huku akichukua tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona.
Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa imesimamishwa kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wakati ligi inasimamishwa Yanga ilikuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 51 kibindoni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ngassa amesema kuwa yupo Mwanza akiendelea na ratiba zake na mpango wa kurudi Dar utakamilika hivi karibuni.
"Nipo Mwanza kwa sasa nikiendelea na ratiba zangu, mpango wa kurudi Dar utakuwa hivi karibuni, kikubwa ni kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ili maisha yarudi kama zamani," amesema.

Post a Comment