EMMANUEL Okwi nyota wa zamani wa Simba anayekipiga ndani ya Klabu ya Al Ittihad anatajwa kurudi Bongo baada ya mambo kuwa magumu nchini Misri.
Nyota huyo raia wa Uganda ambaye anakipiga ndani ya timu ya Taifa lake ni kipenzi cha wana Simba kutokana na mchango wake ndani ya Simba.
Nyota huyo alijiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Misri kwa dau la dola 257,000 zaidi ya shilingi milioni 592 akitokea Simba.
Habari zinaeleza kuwa kushindwa kufurukuta kwa Okwi nchini Misri ni chanzo cha yeye kutaka kurudi kwenye Ligi ya Bongo ambayo ameshaizoea.
"Okwi nyota yake ni Simba ndio maana akiwa hapa huwa anawasumbua wengi lakini kwa sasa mambo huko aliko ni ngumu kutusua ndio maana anafikiria kurudi tena Simba.
"Alishaanza kujenga utawala wake Bongo jambo ambalo linamfanya afikirie pia kurudi ili kurejea kwenye ubora wake kwani haina maana kwamba hana uwezo ila aina ya wachezaji anaokutana nao pamoja na mazingira kumbana," ilieleza taarifa hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema:" Kwa sasa kocha ametoa mapendekezo yake ya mchezaji wa kusajiliwa na kuachwa, hatuwezi kuweka wazi siri za klabu muda ukifika kila kitu kitajulikana,".
Okwi akiwa Simba ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu ikiwa ni msimu wa 2011/12,2017/18 na 2018/19.
Nchini Misri akiwa amecheza mechi 14 ndani ya timu yake hiyo ametupia mabao mawili.
Post a Comment