UONGOZI wa Yanga umesema kuwa Kampuni ya GSM itaendelea kufanya nao kazi kwa kufuata masharti yale yaliyopo kwenye mkataba.
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dr.Mshindo Msolla amesema kuwa wamekubaliana na kuzungumza kwa kina kuhusu namna ya kuendelea kushirikiana katika kazi.
Msolla amesema:"GSM ipo tayari kuendelea kufanya kazi nasi na wapo tayari kuendelea nasi katika shughuli zote kwa mambo ambayo yapo kwenye ishu ya mkataba huku yale mwengine yasiyo ya kimkataba yatasitishwa.
"GSM amekuwa karibu nasi katika ishu ya usajili na mishahara pia alitusaidia kwenye ajira la benchi la ufundi hivyo bado tupo pamoja nasi katika kazi," amesema.
Post a Comment