WILLIAM Lucian, ‘Gallas’ beki wa kulia wa Polisi Tanzania amesema kuwa anaamini kuwa anaweza kuondoka Bongo iwapo atapata nafasi ya kucheza nje ya nchi.
Polisi Tanzania imecheza mechi 29 ina pointi 45 imefunga mabao 29 na safu ya ulinzi imeruhusu mabao 26,ipo nafasi ya sita kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Gallas amesema kuwa malengo yake makubwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na anaamini litawezekana kutokana na uwezo alionao.
"Kipaji nimepewa na Mungu na ninakitumia kutafuta ugali hivyo imani yangu ni kwamba nitapata nafasi ya kuondoka Bongo na kwenda kukipinga nje ya nchi.
"Nina amini kuwa wakati utafika nami nitaishi kwenye ndoto zangu ambazo nimejiwekea, kila kitu kitakuwa sawa wakati ukifika," .

Post a Comment