PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli amesema kuwa amepata dili la kujiunga na moja ya timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Malaysia mambo yakiwa sawa atasepa Bongo.
Nonga anayekipiga Lipuli amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ni miongoni mwa wazawa wanaocheka na nyavu akiwa na mabao 11 na pasi nne za mabao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja umempa nafasi ya kupata timu nchini Malaysia jambo ambalo linampa faraja.
"Ninafurahi kuona kwamba kazi yangu inaonekana na nimepata timu nchini Malysia inashiriki Ligi Kuu nchini humo inaitwa Kuala lumpar FC.
"Muda wa siku 12 nilipata kufanya majaribio na ninashukuru haikuwa mbaya kwani nilionyesha kitu cha kipekee, bado ni mradi endelevu mambo yakiwa sawa nitaweka wazi mipango itakavyokuwa," amesema

Post a Comment