RELIANTS Lusajo, nahodha wa Namungo amesema kuwa anaamini akitua ndani ya Yanga ataendelea kutupia kama kawaida kutokana na uwezo alionao.

Lusajo amekuwa akihusishwa kutua Yanga kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji iliyo chini ya David Molinga mwenye mabao nane ya Ligi Kuu Bara ndani ya Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Lusajo amesema kuwa amekuwa akiskia kuwa anahitajika kutua ndani ya Yanga jambo hilo halimpi presha kutokana na uwezo wake.

"Nina amini kwamba uwezo wa mchezaji huwa haujifichi, iwapo nitapata nafasi ya kurejea Yanga nitaendelea na kasi yangu ya kutupia pale nitakapopata nafasi.

"Uzuri ni kwamba kwa sasa nimezidi kuimarika na kuwa na uwezo wa kufunga jambo ambalo linanifanya niamini kwamba ninaweza kucheza popote ndani na nje ya Bongo," amesema.

Lusajo ametupia mabao 11 na pasi tatu za mabao msimu huu wa 2019/20 kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.