WILLIAN nyota anayekipiga ndani ya Chelsea amewekwa kwenye rada za Juventus na Tottenham ambazo zimetajwa kumuwinda kiungo huyo.

Willian alikuwa akihusishwa kutimka ndani ya Klabu ya Chelsea katika usajili uliopita lakini sasa Juventus wanaonekana kushikilia bango la kutaka kumsajili.

Imeelezwa kuwa nyota huyo anataka kusalia ndani ya London hivyo huenda Spurs wakaipata saini yake.


Kiungo huyo mpaka sasa hana uhakika wa kubaki ndani ya Chelsea baada ya kuambiwa aongeze mkataba wa mwaka mmoja huku yeye hesabu zake zikiwa ni kusaini kandarasi ya miaka miwili.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.