KLABU ya PSG ipo kwenye mpango wa kumalizana na nyota wao Mauro Icard anayekipiga kwa mkopo akitokea Klabu ya Inter Milan.
Raia huyo wa Argentina amekuwa kwenye kiwango chake msimu huu ambapo amecheza mechi 20 na kutupia mabao 12.
Inaelezwa kuwa Juventus nao pia wapo kwenye hesabu za kuipata saini ya nyota huyo ambaye pia mabosi wake AC Milan wameonyesha mpango wa kumrejesha ndani ya klabu yake.
PSG inayoshiriki Ligue 1 kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 27 kibindoni ina pointi 68 huku Milan inayoshiriki Serie A ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 26
Post a Comment