KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba, amefichua kwamba, wakati anakua, alikuwa shabiki mkubwa wa Arsenal na hiyo ilichangiwa na kumfuatilia zaidi Mfaransa mwenzake, Thierry Henry.
Pogba akishangilia na Jesse Lingard ndani ya United |
Mwaka 2009, Pogba alijiunga na United akitokea Le Havre ya nyumbani kwao Ufaransa wakati akiwa na miaka 16, kisha akaondoka na kuelekea Juventus mwaka 2012, akarejea tena Old Trafford kwa uhamisho ulioweka rekodi ya dunia mwaka 2016.
Thierry Henry (kushoto) akishangilia bao na Mfaransa mwenzake, Robert Pires walipokuwa Arsenal |
Pogba raia wa Ufaransa, alisema, Henry alikuwa mchezaji wake kipenzi pamoja na Ronaldinho, Ronaldo na Zinedine Zidane na wakati anaanza soka alitamani kuyafikia mafanikio yao.
"Niwe mkweli kabisa, nilianza kuishabikia Arsenal, hiyo yote ni kutokana na uwepo wa wachezaji wengi kutoka Ufaransa.
"Mimi na ndugu yangu mmoja ndiyo tulikuwa tunaipenda Arsena, lakini mwingine akawa shabiki wa Manchester United.
"Siwezi kusema kingine chochote zaidi ya nilikuwa nampenda Henry na kwa sababu yake nikawa shabiki wa Arsenal.
“Baadaye nikabadilika na kumfuata yule ndugu yangu mwingine ambaye si shabiki wa Arsenal, nikawa naye katika kuishabikia United!"
Pogba akiwa na jezi za Juventus |
Pogba, 27, msimu huu umekuwa si mzuri kwake ndani ya kikosi cha United kwani amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Msimu huu katika Premier amecheza mechi saba tu, hajafunga bao lolote, lakini ana asisti mbili.
Post a Comment